0

 





Na.Dominic Haule 

Mhashamu HENRY MCHAMUNGU Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la DAR ES SALAAM, Amewataka watawa kuishi kwa upendo,unyenyekevu  na Msamaha katika Maisha ya jumuiya Ili kazi ya MUNGU itendeke vizuri.

Askofu Mchamungu Amesema hayo  katika Misa Takatifu ya kuweka Nadhiri za Daima kwa Masista wawili wa  Shirika la Mabinti wa BIKIRA MARIA EMMACURATE (DMI), iliyofanyika  Parokia ya Mtakatifu MARIA KIMARA Mwisho, Jimbo kuu la DAR ES SALAAM.

Amesema miongoni mwa sifa kubwa za utawa ni kujitoa sadaka  kwajili ya wengine na kujishusha na sio  kuwa watu malumbano na kutokuelewana ndani ya jumuiya zao jamboa mbalo alimpendezi MUNGU na ni kinyume na wito wao.

Aidha amewakumbusha watawa hao  kuishi  usafi wa moyo siku zote za Maisha yao ya wito huo  kwani wamejitoa kwajili kanisa na wamejiweka mbali na malimwengu  ambayo yanaweza  kuleta changamoto katika  maisha yao.

Amehitimisha kwa kutoa wito kwa kila mkristo mbatizwa kujitoa kwa ajili ya kuhubiri injili na kumtagaza YESU KRISTO,kwani hilo ni jukumu lao msingi na sio badala yake kwaachia mapadre na masista peke yao.

Pia Amewakumbusha wazazi na Walezi wasio watu wakuwabebesha majukumu ya kifamilia kwa kuwa hao wamejitoa Maisha yao kwaajili ya kulitumikia kanisa na Watu wa Mungu.




Post a Comment

 
Top