Bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa mwezi Juni 2025 imeendelea kushuka na unafuu kwa watumiaji wa vyombo vya moto nchini, ikilinganishwa na bei za mwezi Mei 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati
na Maji (EWURA)
leo 4
Juni 2025, kwa mafuta yaliyopokelewa katika Bandari ya DAR
ES SALAAM, bei ya petroli imeshuka kwa shilingi 72.16,
dizeli kwa shilingi 51.89 na
mafuta ya taa kwa shilingi 184.93.
Kwa bandari ya TANGA,
petroli imeshuka kwa shilingi 69.41 huku dizeli ikishuka kwa shilingi 50.1, na
kwa Bandari ya MTWARA petroli
imeshuka kwa shilingi 71.65 na
dizeli shilingi 51.37.
Aidha, ulinganifu wa bei za mafuta kwa miezi mitatu, Aprili, Mei na Juni 2025, mwenendo umeonesha kuendelea kushuka kwa bei maradufu kutoka shilingi 2,905.34(Aprili) hadi shilingi 2,684.54(Juni) sawa na kupungua kwa shilingi 220.8 petroli iliyopokelewa Bandari ya DAR ES SALAAM.
Post a Comment