Mhashamu
STEPHANO
LAMECK MUSOMBA OSA Askofu wa Jimbo Katoliki BAGAMOYO,
amewataka Wakristo wakatoliki kuwa makini katika kuisikia Sauti ya Mungu
wakiomba msaada wa neema yake ili kuitambua Sauti hiyo na Kuifuata.
Askofu
Musomba ametoa Wito huo wakati alitoa Homilia kwenye adhimisho la Misa Takatifu
ya utolewaji wa Daraja Takatifu ya Upadre kwa Mashemasi wa 4 ambapo 3 ni wa Jimbo
na mmoja ni wa Shirika la Mapendo katika Parokia ya Mtakatifu ANTHONY
wa
PADUA CHUMBAGENI Kanisa Kuu Jimbo Katoliki TANGA.
Aidha
ameongeza kuwa wanapoisikia Sauti ya Mungu na Kuifuata wanakuwa utambulisho wa
Kristo hivyo amewahimiza wawe na unyenyekevu na utii kwa yule aliyewaita
kumtumikia wakitunza utambulisho huo kwa Mungu na kwa Kanisa lake hapa
ulimwenguni kwa kuishi Wito wao na kuwahurumia walionewa na kuvunjika Moyo.
Vilevile
amewataka wazazi na Walezi pamoja na Waamini wote kushirikiana katika Malezi ya
Mapadre hao ili wadumu katika Wito ulioutambulishonwanYesu katika maisha ya
Mwanadamu.
Pamoja
na mambo mengine amewataka Waamini wote kuwasaidia Mapadre katika Safari yako
ya Wito huku akiwataka kuwalea na kuwatumza kwa sadaka na michango yao pasi na
kuwategemea katika kule familia walizotoka kwani wamejitoankwa Bwana na weluwa
Mali ya Kanisa la Mungu.
Misa
Takatifu imeadhimishwa na Mhashamu STEPHANO
LAMECK MUSOMBA OSA Askofu wa Jimbo Katoliki BAGAMOYO
akishirikiana na Mhashamu THOMAS JOHN
KIANGIO
Askofu wa Jimbo katoliki TANGA
na imehudhuriwa na Mapadre. Masista, Watawa wakike na wakiume, pamoja na
Waamini walei kutoka ndani na nje ya Jimbo la Tanga.
Post a Comment