Takukuru mkoa wa
temeke imewakamata watuhumiwa wawili kwa makosa ya kuomba na kupolea
rushwa kinyume na sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na. 11,2017
kifungu cha Na.15, maafisa hao ni wa TRA kigamboni na ustawi wa jamii wa
mahakama ya mwanzo Buguruni.
Manamo tarehe 15
februari, 2018 Bi. Seire Andrea Akilimali, Afisa ustawi wa jamii wa
mahakama ya mwanzo ya Buguruni alifikishwa mahakama ya wilaya ya Temeke
na kufunguliwa kesi namba 136/18 kutokana na mtego ulioandaliwa na na
TAKUKURU na kukamatwa akiomba rushwa ya Tshs.300,00/= na kupokea kiasi
cha Tshs.200,000 ili aweze kumsaidia Mwananchi mmoja ambaye ndugu take
alihukumiwa jela miezi minane ili aweze kupata wepesi wa kutumikia
kifungu cha nje.
Pia tarehe 28
February, 2018 Stratton Sylvester Mutayabarwa Afisa wa TRA kigamboni
alifikishwa mahakama ya wilaya ya Temeke na kufungukiwa kesi Na.180/18
baada ya kupokea rushwa ya Tshs.300,000/= kutoka kwa wananchi mmoja
ambaye ni mmiliki wa bucha ili asimchukulie hatua za kisheria kwa kosa
la kufanya biashara bila kufuata sheria za kodi, hata hivyo kesi zote
mbili zinasikilizwa na watuhumiwa wote Wapo nje kwa dhamana.
Aidha Takukuru
inaemdelea Kuwait had garish wananchi wote kutojihusisha kabisa na
vitendo vya rushwa kwani kushawishi, kuimba na kupokea rushwa yote ni
makosa chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya
mwaka 2017 na atakayebainika kukihusisha na vitendo hivyo vya rushwa
atachukuliwa hatua za kisheria na pia wananchi watoe taarifa kuhusu
vitendo vya rushwa kupitia namba ya bure 113.
Post a Comment