Na.Martin Joseph
Wakuu wa makampuni na taasisi zilizopo hapa nchini wameombwa kuhuzuli mikutano pamoja na makongamano ili iwasaidie kupata fursa za kimaendeleo na hata kuendeleza na kuyainua kiuchumi makampuni pamoja na taasisi zao.
Hayo yemesemwa na mwenyekiti
wa taasisi ya kimataifa ya logistiki
na usafirishaji (CILT) GEORGE MAKUKE alipokuwa akitoa taarifa kwa vyomo vya
habari kuhusu mkutano wa kimataifa wa
taasisi hiyo unaotalajiwa kufanyika Septemba mwaka huu kisiwani Zanzibar.
Amesema kuwa mikutano
pamoja na makongamano mbalimbali ni moja
kati ya sehemu ambazo zimekuwa zikitengeneza
fursa ikiwemo mafunzo pamoja
ajira kwani watu mbalimbali wamekuwa
wakikutana katika sehemu hizo na kubadilisihana mawazo na hata kujengeana uelewa
wa jinsi gani wanaweza wakaziiinua na hata kuzipamaendeleo sekta, kampuni na
hata taasisi zao hivyo basi ni vyema
kuzitumia sehemu hizo kama mahali pakujipatia
fursa mbalimbali.
Wakati huo huo nae
mkuu wa chuo cha mabaria hapa nchini Dkt.ERICK MASSAMI ametoa wito kwa kwa vijana kujifunza mafuzo ya ubaharia ili kuisaidia
nchi kuongeza mapato ya ndani katika
maswala ya usafarishaji wa majini kwani imekuwa ikitumia fedha nyingi kwa
kuwalipa wasafirishaji ambao wanatoka nje ya nchi hivyo hali hiyo imekua
ikipelekea hata kiwango cha mapato ya
nchi kushuka.
Post a Comment