Waamini
Wakatoliki wamealikwa kujifungamanisha na Mungu ili kumruhusu Mungu atawale
maisha yao.
Hayo
yamesemwa na Mhashamu TITUS MDOE Askofu
wa Jimbo Katoliki Mtwara wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya
Miaka 50
ya Parokia ya Mtakatifu PAUL MAJENGO
jimboni MTWARA.
Katika
homilia yake Mhashamu Mdoe amewahimiza waamini wa Parokia hiyo kuwa na imani
thabiti ili kuweza kumtangaza Mungu popote bila ya woga ikiwa ni pamoja na utii
wa kweli unyenyekevu na matumaini kwa Mungu aliye Baba wa haki na upendo.
Kadharika
amewasisitiza waamini hao kufuata mfano wa mama BIKIRA
MARIA
kwa kuonesha upendo kwa jirani na kuwahudumia wa hitaji kwa haraka kwa kufanya
hivyo ni kuiishi imani kwa matendo.
Wakati
huohuo mara baada ya Adhimisho la Misa Takatifu Mhashamu Mdoe akizungumza na
waandishi wa habari amewashukuru waamini kutenda matendo ya huruma na huduma
hasa kipindi hiki cha Jubilei na kuwa watu wa shukrani kwa Mungu na
wanadamu.
Post a Comment