
Na.Martin Joseph
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro leo amemuapisha Kamishna wa Polisi CP Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar baada ya kuteuliwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania
na amiri jeshi mkuu Dkt John Pombe Magufuli
Hafla hiyo ya kuapishwa Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Haji imefanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam
na kuhudhuriwa na makamishina na maofisa wakuu waandamizi wa jeshi la polisi kutoka
Tanzania bara na Zanzibar.
Kufuatia kiapo cha utii mbele ya Inspekta Jenerali
wa Jeshi la polisi Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mohamed Hassan Haji amesema
vipaumbele vilivyotolewa na viongozi wa juu pamoja na maelekezo yote atahakikisha
anayashughulikia kwa wakati ili watanzania waishi kwa amani.
Nae Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro
amesema,vyombo vya ulinzi na usalama vinashirikiana kwa amani na huku akieleza
kuwa Zanzibar changamoto pekee iliyobaki
ni ajali za barabarani na hivyo watahakikisha wanakabiliana na wavunjifu wa
kanuni na sheria za barabarani.
Ikumbukwe kuwa CP Mohamed Hassan Haji alijiunga na Peshi
la Polisi mwaka 1991 na kupandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Mkaguzi wa Polisi,Mrakibu
Msaidizi wa Polisi,Mrakibu wa Polisi,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi,Kamishna
msaidizi wa Polisi hadi Kamishna wa Polisi na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi
Zanzibar.
Post a Comment