
Na.Martin Joseph
Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh, Dkt.JOHN POMBE
MAGUFULI amemtengua aliyekua mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya BUTIAMA
Bw.SOLOMON NGILIULE kwa kinachosadikiwa kuwa ameshindwa kusimamia ipasavyo
maeneo yake ya kazi.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari waziri wa ofisi
ya Raisi Tawala za Mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Mh.SELEMANI JAFO amesema
kuwa utenguzi huo umefanyika baada ya kufanyika kwa ziara ya kikazi ya Waziri
mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.KASSIM MAJALIWA ambapo imebainika
wazi kuna watendaji walio chini ya baadhi ya Halmashauri kushindwa kusimamia
vyema maeneo yao ya kazi.
Hivyo basi kutokana na hali hiyo ikapelekea Mh.Raisi
Dkt.JOHN POMBE MAGUFULI ambaye pia ni mwenye dhamana ya Ofisi ya TAMISEMI
kumtengua kiongozi huyo wa halmashauri hiyo Pia waziri JAFO amemwelekeza katibu
mkuu wa wizara hiyo kuwa hamchukulie hatua stahiki mweka Hazina aliyehusika wakati wa matumizi
hayo mabaya ya fedha za seraikali yaliyofanyika hapo awali.
Aidha amewataka watendaji wote walio chini ya Tawala za
Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia
kanuni za utumishi wa umma na kuahakikisha rasiliamali za Nchi zinatumika kwa
maslahi mapana ya Wananchi na Taifa kiujumla.
Post a Comment