Na.Vedasto George,Morogoro
Kampeini ya moro yetu safi imetekelezwa hileo mala baada ya wananchi na wakazi wa kata ya mazimbu mkoani Morogoro kujitikeza kwa wingi katika zoezi la kufanya usafi katika eneo linalo jengwa zahanati ya kata mkoani humo.
Akizungumza mala baada ya kumaliza zoezi la usafi mkuu wa wila ya morogoro mjini Bi. Regina Chonjo amewashukulu wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo na kuwaomba wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayo weza kujitokeza ikiwemo kipindu pindu.
Aidha Bi. Chonjo amewataka wananchi wote mkoani humo walio na viwanja vikubwa ambavyo avijaendelezwa kama inavyo takiwa waviendeleze mala moja ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwemo kunyangaywa viwanja hivyo.
Katika atua nyingine mkuu wa wilaya ya morogoro Bi. Chonjo amewataka viongozi wa kisiasa mkoani humo kuacha mala moja kuwapotosha wananchi juu ya masuala ya maendeleo na kusema kuwa siasa itumike kwa kuleta maendeleo.
Awali akimkalibisha mkuu wa wilaya Mhe. msitaiki meya na diwani kata ya mazimbu Bw. Paschal Kihanga amebainisha kuwa zoezi la usafi katika kata iyo niendelevu na kuwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kila mwisho wa mwezi kufanyausafi ili kuiweka morogoro safi.
Post a Comment