
MWANASOKA nyota wa Brazil, Ricardo Izecson dos Santos Leite 'Kaka; ametangaza rasmi kustaafu.
Kaka
mwenye umri wa miaka 35 sasa, msimu uliopita alichezea Orlando City ya
Ligi Kuu ya Marekani (MLS) na alisema atastaafu mwishoni mwa msimu.
Mbrazil huyo alicheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Colombus Crew mwezi Oktoba - mchezo ambao timu yake ilifungwa 1-0.
Tangu
hapo haikuwekwa wazi kama Kaka atarudi kucheza mechi moja ya kuaga na
timu yake ya taifa, Brazil, au atastaafu moja kwa moja mchezo alioupenda
maishani mwake.
Lakini jana ameposti kwenye mtandao wa kijamii kuweka wazi hilo.
Aliposti
picha yake isiyo ya rangi akiwa amevaa fulana yake maarufu 'Mimi ni wa
Yesu' aliyoionyesha kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya
Liverpool, Kaka ametoa taarifa juu ya mustakabali wake.
'Baba,
Ilikuwa zaidi ya nilivyofikiria. Nakushukuru! Sasa niko tayari kwa
safari nyingine. Katika jina la Yesu. Amin,"ameandika Kaka.
Post a Comment