
Kikosi cha Yanga kimetua salama Mjini Mwanza tayari kwa pambano lake la Jumapili dhidi ya wenyeji Mbao FC, Mpambano wa Ligi Kuu ambao utachezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Kocha msaidizi wa timu hiyo Shadrack Nsajigwa amesema, timu imewasili salama na leo wanatarajia kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Kirumba, pamoja na kesho kabla ya kujiandaa na mchezo huo ambao wameupa umuhimu mkubwa.
“Nashukuru tumewasili salama Mwanza, hali ya hewa ni nzuri na kufika mapema siku mbili kabla ya mchezo kutatusaidia kufanya vizuri kwenye mchezo wetu wa keshokutwa kwasababu tumedhamiria kushinda mchezo huo ukizingatia Mbao ni timu nzuri na imeuwa ikitusumbua sana,” amesema Nsajigwa.
Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ikiwa na pointi 21, huku mahasimu wao Simba wakiwa ndiyo vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 23 huku Azam FC wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi sawa na Simba.
Post a Comment