
Straika
wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa, ametoa kali ya aina yake kwa
kusema kuwa haoni tofauti yake na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo kwa kuwa wote wameshindwa kufunga mabao ya kutosha msimu huu na
hajui ni kwa nini.
Mussa
ambaye aliibuka mfungaji bora msimu uliopita kwa kufunga mabao sawa na
mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simon Msuva, aliyetimkia Morocco, mpaka
sasa amefanikiwa kufunga bao moja katika mechi alizocheza, akizidiwa
mabao saba na kinara wa ufungaji katika ligi ya msimu huu, Mganda
Emmanuel Okwi.
Mussa
alisema kuwa kupitwa mabao katika ligi ya msimu huu, hakuwezi
kumkatisha tamaa ya kuvunja rekodi yake kwa kuwa hata Ronaldo ameshindwa
kufanya hivyo kwenye ligi ya Hispania msimu huu kwani amefunga mabao
manne tu mpaka sasa.
“Kiukweli
kwamba ligi ya msimu huu ni ngumu, ushindani umekuwa mkubwa, najaribu
kupambana kuona naweza kufunga vipi lakini siwezi na sijui kwa nini,
siyo kwamba nafurahia hali hii kwa sababu bado nataka kufikia rekodi
yangu ya msimu uliopita.
"Unajua
siku zote mshambuliaji anatakiwa afunge na kitu ambacho nataka
kiendelee kwa upande wangu maana kwa sasa naona sioni tofauti yangu na
Ronaldo kwani hata yeye amekuwa anashindwa kufunga mabao na kufikia
rekodi yake ya msimu uliopita hivyo watu wajue siyo kwamba nafurahia
hali hii," alisema Mussa.
SOURCE: SALEHE JEMBE
Post a Comment