
Michuano ya Australian Open imeanza rasmi chini Australia ambapo Mswiss Roger Federer ameanza vyema michuano hiyo kwa kumpiga Marton Fucsovics raia wa Hungary na kutinga robo fainali.
Federer ambaye ni mshindi wa Grand Slam kwa mara 19 alimfunga Fucsovics ambaye anashika nafasi ya 80 katika viwango vya tennis duniani kwa seti tatu mfululizo 6-4 7-6 (7-3) na seti 6 kwa 2.
Matokeo haya ya Federer yanamfanya Federer kukutana na raia wa Czech Tomas Berdych katika hatua ya 8 bora, Federer na Berdych walishakutana mwaka jana pia ambapo Federer alimtoa Berdych.
Akizungumzia mchezo ujao Federer amesema ana uhakika Berdych atataka kulipiza alichomfanya mwaka jana na anaamini mchezo ujao unaweza kuwa mgumu sana kuliko mchezl uliopita.
Post a Comment