Watumiaji wa bima wanoanunua bidhaa kutoka nje ya nchi wametakiwa
kukata bima kupitia makampuni ya ndani ya nchi na sio badala yake kukatama bima
kutoka katika makampuni ya nje ya nchi
kwani kuifanya hivyo kutasaidia kuongezeka kwa mapato ya ndani na hata
kupelekea kasi ya
kukua kwa uchumi kuongezeka uchumi hapa nchini.
Hayo yamesemwa na kamishina wa bima kutoka mamlaka ya usimamizi wa shuguli za bima Bw.BAGHAYO SAQWARE
alipokuwa akifungua semina ya mafunzo kuhusu utumiaji wa mfumo wa kununua bima
kupitia matandaoni (TIIP) kwa waandikishaji wa bima kutoka katika makampuni
mbalimbali hapa nchini.
Amesema kuwa serikali imekua ikitoa fedha yingi kulipa
makampuni ya bima yaliyopo nje ya nchi kwani watumiaji wengi wa bima wanaoagiza
bidhaa kutoka nje ya nchi wamekuwa
wakikata bima kutoka katika makampuni ya nje hivyo hali hiyo imekuwa ikichangia
kushuka kwa mapato katika makampuni ya
bima hapa nchini na hata kupelekea mapato mengi kutoingia serikali hivyo hali
hiyo inaweza kusababisha kasi ya kukua kwa uchumi kupungua.
Pia SAQWARE ameeleza
kuwa ni muhimu makampuni na watu binafsi
wanaotumia bima kuutumia mfumo wa
kukunua bima kupitia matandaoni(TIIP) kwani wasio fanya hivyo watakuwa
wanakwenda kinyume na sheria ya bima ya mwaka 2009.
Hivyo basi kamishina wa bima anaweza kuwapa adhabu kwa
mujibu wa sheria ikiwemo kufutiwa leseni,faini au kosa hilo likijumuishawa
katika kuhujumu uchumi itapelekea kujumuishwa katika makosa ya jinai
kwaiyo ni muhimu kuutumia mfumo huo
kwani unafaida nyingi kwa watumiji wa bima na Taifa kiujumla.
Aidha nae Raisi wa taasisi ya bima Tanzania(IIT) Bw.BOSCO
JAMES amesema kuwa mafunzo hayo kwa waandikishaji wa bima yamelenga
kuwaelimisha jinsi ya kutunza taarifa za watumiaji wa bima kupitia matandao
hivyo taasisi hiyo ya IIT kwa kushirikiana na chama cha wakala wa bima Tanzania(TIBA)
pamoja na Mamlaka ya usimazi wa shuguli za bima Tanzania (TIRA) wameshirikiana
kuaandaa semina hiyo ili kuwapa uelewa waandikishaji hao. lengo likiwa nikutoa
mafunzo yatakayowasidia waandikishija wa bima katika makampuni mbalimbali kujua
jinsi gani ya kuutumia mfumo huo ili
waweze kuelewa jinsi gani ya
kuwaandikisha watu wanaoagiza mzigo kutoka nje ya nchi na kutunza taarifa zao
na kufikisha katika mamlaka zinazo husika ili kufanya watumiaji wa bima kukunua
bima kutoa ndani ya nchi.
Post a Comment