0








Image result for vedast makota




Na.Martin Joseph

Jamii imetakiwa kujua kuwa utupaji wa taka kiholela hasa taka ngumu pasipo kufuata utaratibu ni moja kati ya vitu vinavyosabisha magonjwa katika jamii,mafuriko na hata kupelekea kuzalisha gesi ambazo zitakuwa na madhara kwa maisha ya viumbe hai hasa hasa binadamu.

Hayo yemesemwa na Kaimu  Mkurugenzi wa baraza la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) Dkt.VEDAST MAKOTA alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa kuandaa mkakati wa kitaifa wa kusimamia taka Tanzania ulioandaliwa na shirika la umoja wa mataifa la kusimamia  mazingira (UN environment) uliyofanyika Jijini DAR ES SALAAM.

Amesema kuwa   kumekuwa na tabia ya kutupa taka pembezoni  mwa  barabara kwenye miferejini na hata sehemu nyingine hivyo hali hiyo imekuwa ikileta madhara makubwa katika jamii  na hata kuhatarisha maisha ya viumbe hai  mbalimbali hivyo ni vyema jamii ikatumia utaratibu mzuri katika kutupa taka na hata kutunza mazingira.

Aidha  nae mwenyekiti wa taasisi isiyo kuwa ya kiserikali inayojishulisha na utuzaji wa mazingira hapa nchini (AGENDA) ambaye pia ni kiongozi wa mradi wa kusimamia taka ngumu Prof.JAMIDU KATIMA ameiomba serikali kuendelea kushirikiana na wadau pamoja na taasisi mbalimbali zinazojishulisha na maswala ya  mazingira hapa nchini kwani kwakufanya hivyo kutalinusulu taifa kuondokana na madhara ambayo yanatokana na uchafuzi wa mazingira.

Post a Comment

 
Top