0





 

 
 Related image

 Na.Martin Joseph
Benki kuu ya dunia imehahidi kutoa Dola millioni 300 kwa serikali  ya Tanzania kupitia wizara ya maji na Umwagiliaji  fedha hizo zimetolewa kwa lengo la  kuboresha  miradi mbali mbali   ya maji safi na salama maeneo ya vijijini hapa nchini.

Hayo yamesemwa na  Naibu wa waziri wa Wizara ya maji na umwagiliaji JUMAA AWESO alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini DAR ES SALAAM baaada ya kumaliza kikao kilicho andaliwa na benki kuu ya dunia kwakushirikaiana na wizara hiyo  ambacho walikua wakijadili ni namna gani wanaweza kuwapatia watu maji safi na salama.

Amesema kwasasa kumekuwa na vituo vichache ambavyo vimekuwa vikitoa maji kwani vituo vingi vimeshindwa kutoa maji kutokana na sababu za kiufundi ambapo waandisi wengi wamekuwa wakibuni miradi ya maji kipindi cha mvua ambapo kipindi hicho uhaba wa maji unakuwa mdogo na watu wengi wamekuwa wakitumia maji ya mvua hivyo kwa kipindi cha kiangazi miradi mingi huwa inashindwa kutoa maji kutokana na kukaushwa na jua.

Kwaiyo hali hiyo imekuwa  ikiwafanya wananchi wengi  hasahasa wa vijijini  kuwa na uhaba wa maji  hivyo ameeleza kuwa endapo fedha hizo zitapatikana ataakikisha kuwa anazitumia vizuri kwakukamirisha miradi mbalimbali ambayo ilikuwa bado ajikamilika na ataakikisha kuwa miradi hiyo itabuniwa kipindi cha kiangazi na watakao fanya kazi hiyo watakuwa waandisi kutoka hapa nchini kwani wao kwaasilimia kubwa ndio wanajua shida za maji zilizopo hapa nchini.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira kwaajili ya kuvisaidia vyanzo vya maji visikauke na hata kupelekea maeneo mbalimbali kuepukana na uhaba wa maji.

Post a Comment

 
Top