
Mkufunzi wa Brazil Tite amesema timu
yake bado inatatizwa na "mizimu" ya kipigo cha 7-1 ambacho walipokezwa
na Ujerumani katika nusu fainali ya Kombe la Dunia miaka minne
iliyopita.
Mataifa hayo mawili yatakutana tena wka mara ya kwanza
Jumanne mjini Berlin tangu Brazil walipoaibishwa kwao nyumbani wakati wa
michuano hiyo ya Kombe la Dunia."Hii ina maana kubwa sana kisaikolojia - hakuna anayehitaji kujidanganya kuhusu hilo," Titea aliambia jarida la Kicker.
"Matokeo hayo ya 7-1 ni kama mizimu, watu bado huyazungumzia. Kadiri unavyoyazungumzia zaidi, ndivyo mizimu hii inavyochukua muda mrefu kutoweka."
Toni Kroos alifunga mabao mawili wakati huo naye Miroslav Klose akavunja rekodi ya ufungaji mabao Kombe la Dunia mwaka 2014 Ujerumani walipoafanikiwa kujiweka mbele 5-0 dakika 29 za kwanza kwenye nusu fainali hiyo.
Katika mechi hiyo ya kimataifa ya kirafiki itakayochezewa Berlin, kiungo wa kati wa Manchester City Fernandinho anatarajiwa kuingia uwanjani nafasi ya Douglas Costa.
Hilo litakuwa ndilo badiliko pekee kwenye timu ambayo ililaza Urusi 3-0 mjini Moscow mnamo Ijumaa bila nyota wao Neymar ambaye anauguza jeraha.
Post a Comment