0
Imeelezwa  kuwa wauguzi na wakunga hapa nchini wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbaliikiwemo kupatwa na matatizo ya kuumwa mgongo hivyo hali hiyo imekuwa ikiwafanya kushindwa kufanya kazi kwa muda mrefu kama inavyotakiwa.
Hayo yamesemwa na mkurugezi wa huduma za uuguzi na wakunga kutoka wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsi,wazee na watoto GUSTAV MOYO alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa linalojishulisha na idadi ya watu(UNFPA) kuhusu kongamano la kisayansi la wauguzi na wakunga linalotarajiwa kufanyika Aprili Nne na tano mwaka huu mkoani DODOMA huku mgeni rasmi katika kongamano hilo akitarajiwa  kuwa waziri wa wizara hiyo UMMY MWALIMU.
Amesema kuwa hapa nchini bado  kuna uhaba wa wakunga na waguzi  hali ambayo imekuwa ikichangia  mkunga mmoja  kuhudumia idadi kubwa ya akina mama wajawazito kwa siku bila kupumzika na muda mwingine mwingine hali hiyo imekua ikiwasabibshia wakunga hao kuiona kazi hiyo kuwa ngumu hata  kuchukua hatua ya kuacha kzai ya ukunga.
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha wakunga Tanzania-TAMA, Dkt. SEBALDA LESHABARI ameeleza kuwa kazi ya ukunga ni moja kati  ya kazi ambazo zinahitaji moyo kwani watu wengi hasa hasa wanawake  wamekua wakiimbia kazi hiyo kutokana na mazingira ya kazi kuwa magumu hali ambayo inachangia kuongezeka kwa vifo vya akina mama wajawazito na watoto wakati ama kabla ya kujifungua.
Hivyo ametoa wito kwa serikali na wadau wa afya kutengeza mazingira mazuri ambayo yanaweza  kuwavutia watu wengine waweze kuingia katika kazi hiyo kwani endapo wakunga wataongezeka hapa nchini inaweza ikasaidia kupunguza vifo  vya  mama na mtoto.
 Pia ameeleza kuwa ni vyema wananchi wakatambua kuwa taaluma ya ya ukunga ni moja kati ya taaluma ambazo zinatakiwa kuheshimika kwani watu wanaotakiwa kuingia katika taaluma hiyo ni wale wenye ufaulu mzuri na sio badala yake kuwa na watu wasio na ufaulu mzuri kwa watukua wanatoa huduma ambazo hazitakuwa bora kwa wagonjwa.
 

Post a Comment

 
Top