0

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025 / 2026, jijini DODOMA leo Mei 28, 2025.

Waziri KOMBO ameliomba bunge lipitishe bajeti hiyo ambayo ni kiasi cha shilingi Bilioni 340.5 ikiwa na vipaumbele vitano.

Aidha amewataka wabunge kutumia fursa ya kuzungumza na mabalozi waliofika nchini kwa ajili ya mkutano wa diplomasia ili kuwasaidia kupata wawekezaji katika miradi  mbalimbali ndani ya majimbo yao.

Kadhalika waziri KOMBO  amezitaka sekta binafsi nchini kushiriki  kuchangia fursa zitokanazo na diplomasia kiuchumi kupia uwili yaani kikanda na kimataifa kwani ufanya hivyo itasaidia kutoa ajira kwa vijana wengi wa Kitanzania.

Amehitimisha kuwa Jumla ya wataalam kumi na saba kutoka nchini QATAR wamekuja TANZANIA kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa madereva ambapo katika mafunzo hayo watapata kupewa ujuzi wa kufahamu magari yanayoendeshwa kidijitali.




 

 

 

 

Post a Comment

 
Top