Serikali
imeingia makubaliano na nchi mbalimbali ili kurahisisha utaratibu wa viza
ambapo raia wa nchi 71
hawahitaji viza wanapoingia nchini.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa maliasili
na utalii DUNSTAN
KITANDULA, alipokuwa akijibu swali la Mbunge Dkt. Pius STEPHEN
CHAYA,aliyetaka
kujua ni jitihada gani zimefanyika kurahisisha upatikanaji wa VISA
kwa Watalii wenye uraia tofauti wanaokuja nchini.
Amesema Serikali imeendelea kuboresha utaratibu wa
utoaji wa viza nchini ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani ambapo
kupitia Idara ya Uhamiaji imeanzisha
mfumo wa maombi ya viza kwa njia ya mtandao (e-Visa)
unaowawezesha watalii kuomba viza popote walipo duniani.
ameongeza kuwa Serikali imeboresha Kanuni za Uhamiaji za mwaka 2023
(GN 428)
ambapo kwa sasa watalii wanaotumia Visitors
Pass
wanaruhusiwa kutembelea Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kurejea
TANZANIA
bila hitaji la kuomba upya pasi ya kuingia nchini.
Post a Comment