
Bado
hakujawa na uhakika wa wachezaji wapya taarifa zao kusajiliwa kwenye
mtandao wa usajili wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Taarifa zinaeleza ahadi sasa, mtandao huo haujawa tayari na wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo hawajasajiliwa.
Imeelezwa, bado wataalamu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wamekuwa wakiendelea kuoambana kutaka mambo yawe safi.
Baadhi
ya wachezaji waliokwamishwa na TMS ni wale wa Simba, Asante Kwasi
anayetokea Lipuli ya Iringa na Dayo Domingues kutoka Ferreviario ya
Msumbiji.
Awali
TFF, ililazimika kulifungua tena dirisha dogo baada ya mtandao huo
kuleta matatizo. TFF ilisema imelifungua dirisha kwa saa 24 lakini hadi
sasa, bado mambo ni mabaya.
Post a Comment