
Msemaji wa Simba, Haji Manara amekutana na wakati mgumu baada ya kuzushiwa kifo.
Baadhi ya watu wametupia mtandaoni wakielezea kuwa Manara amefariki dunia.
Hata hivyo, Manara amezungumza na waandishi na kusema taarifa hizo ni uzushi mkubwa na alikwenda msibani na kupokelewa kwa shangwe kwa kuwa tayari watu walipata taarifa kwamba amefariki dunia.
"Jaman
ndugu zangu toka Jana kuna habari znazagaa kuwa nimekufa. Kaka yangu
anaitwa Ramadhan kitenge alinipigia Jana kuwa kaona fb," anaelelezea
Manara.
"Ndugu
zangu na mama yangu mzazi nao walipigiwa simu, nikapuuza. Lakini leo
wakati nikijiandaa kwenda msibani kwa mwanachama wetu maarufu dada Fii
kambi.
"Nikapigiwa
cm nyingi za kutaka kujua hali na uhai wangu na kweli nilipofika
msibani nimekuta vilio vya kina mama kuwa nimefariki.
"Kiukweli
mm ni mzima wa afya, siumwi chochote na Alhamdulillah naendelea na
shughuli zangu kama kawaida. Kufa tutakufa tu kwa ahadi yake Mungu,
puuzeni
Post a Comment