
Klabu ya Azam FC imeendelea kuingia kwenye neema mpya baada ya kuingia tena mkataba mpya wa Benki ya wazalendo ya NMB.
NMB wanaonekana kufurahishwa na mambo yalivyokwenda katika mkataba wao wa kwanza na NMB baada ya kuonekana kuutendea haki mkataba wao wa awali wa benki hiyo hivyo imewaongezea mwingine wa mwaka mmoja ambao utawasaidia kupambana kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Akizungumza wakati wa kusainishana mkataba huo Mkurungezi wa NMB, Imeko Bussemaker, alisema kwamba wameamua kuingia mkataba mpya na Azam FC.
Bosi huyo ameweka wazi namna ambavyo wamevutiwa na Azam FC na namna walivyoheshimu mkataba wao.
Wanaamini
Azam itaongeza wigo mkubwa katika kuzalisha wachezaji wachanga hapa
nchini ambao wataiinua hata timu ya taifa wanayoidhamini pia.
Naye,
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed, yeye amewashukuru NMB kwa
udhamini huo “Niwashukuru sana kwa hili lakini huku napenda niwaahidi
kua siku chache zijazo nitarudi hapa tena kuwakabidhi Kombe la Ligi Kuu
Bara.
"Kwani tunaamini hadi mwisho
wa msimu mambo yatanyooka maana farsafa yetu kwa sasa tunaendelea
kupambana kimyakimya kama tunamfukuza mwizi,” alisema Abdul.
Post a Comment