Ligi
ya Wanawake ya Serengeti Premier Lite hatua ya nane bora inatarajia
kuanza kutimua vumbi Februari 24, 2018 kwenye viwanja vinne.
Mchezo kati ya Kigoma FC na Simba Queens utakaochezwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika ndio utakuwa mchezo rasmi wa ufunguzi.
Mechi
nyingine zitakazochezwa katika siku hiyo ya ufunguzi ni Panama
watakaokuwa nyumbani Uwanja wa Samora kucheza na Evergreen,JKT Queens
wakicheza dhidi ya Alliance kwenye uwanja wa Mbweni.
Mechi nyingine ni ile itakayowakutanisha Baobab na Mlandizi Queens itakayochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kabla
ya kufika kwenye hatua hiyo,ligi hiyo inayodhaminiwa na bia ya
Serengeti Premier Lite kinywaji murua na chenye ubora wa juu ilianzia
kwenye hatua ya makundi ikichezwa kwenye Kituo cha Dar Es Salaam
kilichotumia Uwanja wa Karume na Kituo cha Arusha kilichotumia Uwanja wa
General Tyre.
Post a Comment