Wananchi wametakiwa kupewa elimu juu ya kujikinga na ajali
za barabarani kwani kufanya hivyo itasaidia kupunguza idadi ya ajali za
barabarani na hata kupunguza kwa kiasi kubwa
ongezeko la wagonjwa wanavunjika viungo Mahospitalini.
Hayo yamesemwa na Dkt.bingwa wa mifupa na mishipa amabaye pia ni kaimu mkurugenzi wa kitengo cha Moi muhimbili
Dkt.SAMWELI SWAI alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu njia
zinazotumika katika kuwatibu watoto wenye matatizo ya vichwa,migongo wazi na
waliopata ajali na kuvunjika viungo.
Amesema kumekuwa na
ongezeko kubwa la wagonjwa katika kitengo hicho walivunjika viungo kutokana na ajali za barabarani hasa hasa waendesha pikipiki maarufu kama boda
boda kwani wamekuwa wakizadharau sheria za barabarani na elimu zinazotolewa na vyombo mbalimbali vya usalama
ikiwemo kitengo cha usalama barabarani pamoja na vyombo vya habari.
Hivyo basi Dkt.SAMWELI ameeleza kuwa kitengo hicho cha Moi kwakushirikiana na vyombo mbalimbali vya
usalama barabarani waatakikisha kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili
kupunguza kabisa tatizo la ajali za
barabarani.
Wakati huo huo
taasisi ya moyo ya jakaya kikwete(JKCI)kwa kushirikaiana na taasisi ya Okoa
Moyo wa mtoto(SACH) wameweka kambi ya siku tano katika Hospitali ya taifa ya muhimbili kwa lengo la kufanya
upasuaji wa bila kufungua kifua kwa watoto,uchunguzi wa moyo kwa watoto,utohaji
elimu ya upasuaji wa moyo bila kungua kifua na jinsi ya kuwa hudumia watoto
waliofanyiawa upasuaji huo.
Taarifa kutoka katika taasisi hiyo zinaeleza kuwa mbaka sasa watoto 15 wenye
matatizo ya moyo wameshafanyiwa upasuaji na watoto 32 wamefanyiwa uchunguzi wa
moyo ambapo watoto 20 wamefanyiwa matibabu katika kambi hiyo na wenngine 12
waliobaki watatibiwa na madakatri wa ndani kuanzia wiki ijayo.
Post a Comment