
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limefanya ukaguzi wa viwanja
vinavyotumika kwa kombe la Shirikisho na kuzuia viwanja vitatu kutumika
kwa mechi zinazofuata za hatua ya raundi ya tatu kwa kutokidhi kiwango
kinachotakiwa.
Viwanja
ambavyo havitaweza kutumika kwa raundi hiyo ya tatu ni pamoja na Uwanja
wa Nachingwea unaotumiwa na Majimaji Rangers ambao watalazimika kwenda
Ilulu Lindi kucheza mchezo wake na Mtibwa Sugar kwenye raundi hiyo.
Uwanja
mwingine ni uwanja wa CCM Mkamba Morogoro unaotumiwa na timu ya Shupavu
nao hautatumika kwa raundi hiyo na badala yake Shupavu watautumia
Uwanja wa Jamhuri Morogoro kwa mchezo wake na Azam FC.
Nayo
timu ya Ihefu ya Mbarali haitatumia Uwanja wake kwa raundi ya tatu
dhidi ya Yanga na badala yake mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine Mbeya.
Post a Comment