0





 Mahakama ya Tanzania  pamoja na wadau muhimu katika sekta ya Sheria  wamewataka wananchi kuhudhuria maadhimisho ya wiki ya sheria nchini  kwa lengo la kufikia Dira ya Upatikanaji wa  haki kwa wakati.

 Akizungumza Na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam  Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma  ameeleza kuwa  kwa mujibu   wa Ibara ya 107A  ya  katiba imepewa Mamlaka ya mwisho katika utoaji haki,hivyo huadhimisha siku  ya Sheria itakuwa tarehe 1 februari mwaka huu ni siku maalum ambayo itaashiria kuanza rasmi kwa shughuli za mahakama kwa mwaka huu.
Jaji Mkuu Ibrahim ameweza kubainisha kuwa Mahakama ya Tanzania  pamoja  na wadau muhimu katika Sekta ya sheria watatumia siku tano  kuanzia tarehe 27 hadi 31 Januari mwaka huu kutoa elimu yaSheria kwa wananchi watakaopata nafasi ya kuhudhuria.
Wakati akizungumzia  swala hili ameitaka jamii kuzifahamu  shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mahakama pamoja na wadau wa Sekta ya Sheria  ili kufikia Dira ya upatikanaji wa haki kwa  wakati.

Aidha,Jaji Mkuu Ibrahim ametoa  wito na kusisitiza kuwa Wananchi na wadau wote wa Sheria wanaombwa kutembelea  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwaajili ya kujifunza na kupata huduma mbalimbali za kisheria kutoka kwa majaji,mahakimu,wasajili watendaji,Mawakili wa serikali na Mawakili wanaojitegemea ambao watakuwa tayari kuwasikiliza na kuwahudumia ipasavyo.

Post a Comment

 
Top