
Na.Mwandishi Wetu
Baraza la madiwani Dar es salaam
limefanya kikao ambacho ni kikao cha kawaida cha robo ya mwaka ambacho
kimeongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo Isaya Mwita ambapo
zimejadiliwa ajenda mbalimbali zinazohusu maendeleo ndani ya jiji la Dar
es salaam.
Moja ya hoja
iliyowasilishwa ni kuhusu mapato yanayopatikana ndani ya soko la
kariakoo ambapo imeonekana kuwa soko hilo limekuwa likisababisha hasara
kubwa sana ndani ya mapato ya jiji la Dar es salaam.
Akichangia hoja hiyo diwani kutoka kinondoni Abdallah Mtinika amesema kuwa soko hilo limekuwa na changamoto nyingi kwa Kipindi kirefu lakini hakuna ufumbuzi wowote uliopatikana na kuomba mwenyekiti wa Baraza kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo.
“Soko la kariakoo
limekuwa likisababisha hasara kubwa kila mwaka na hakuna ufumbuzi
uliopatikana hivyo tunaomba mwenyekiti utolee ufafanuzi jambo hilo”
amesema Mtinika.
Kwa upande wake mwenyekiti akijibu hoja hiyo amesema kuwa suala hilo wameshaliongelea na imebainika kuwa ni kweli soko hilo limekuwa likisababisha hasara kubwa sana na kuongeza kuwa wameshaongea na uongozi wa kariakoo na umeahidi kufanya maboresho na mabadiliko ndani ya soko hilo.
Pia mwenyekiti amesema kuwa wameamua kuwapa muda wakuu wa masoko la kariakoo ili waone utendaji wao kwani uongozi huo umeahidi kuja na mabadiliko makubwa kwa mwaka huu sambamba na kuonyesha ripoti ya mapato yanayopatikana ndani ya soko.
Post a Comment