Mmoja
wa wanachama wakongwe wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema
kuwa ataendelea kupinga suala la ukodishwaji wa klabu hiyo hadi
atakapoingia kaburini na kudai kuwa wanachama waache kumsakama kwa kuwa
Serikali ndivyo ilivyoamua.
Hivi
karibuni Klabu ya Yanga ilitangaza kuanza mchakato wa mabadiliko kama
ilivyo kwa watani wao Simba ambao wamemkabidhi timu Mohamed Dewji ‘Mo’
kwa ajili ya kuingia katika mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu kwa njia
ya hisa.
Akilimali
amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa miongoni mwa wanachama ambao
wanapinga mabadiliko ndani ya klabu hiyo jambo ambalo limekuwa
likiwachukiza baadhi ya wanachama.
Akilimali
alisema kuwa, amekuwa na bahati mbaya kwa baadhi ya wanachama na
viongozi wa Yanga kutokana na kupinga suala la Yanga kumilikiwa na mtu
mmoja na kudai kuwa ataendelea kufanya hivyo hadi atakapoingia kaburini.
“Nimekuwa
na bahati mbaya kwa baadhi ya wanachama na viongozi, ni kutokana na
kukataa katu suala la Yanga kumilikishwa mtu mmoja hilo haliwezekani na
nitapinga hadi naingia kaburini.
“Nipo
tayari uanzishwe mfumo wa kampuni kama inaavyotajwa katika katiba ya
Yanga ibara ya 56 ambayo inasema Yanga itaanzisha kampuni ya umma ambapo
wanachama wanamiliki hisa asilimia 51 na wanahisa asilimia 41.
“Lakini
kwa kuwa nilikataa ndiyo naambiwa napinga mabadiliko, Yanga haikodishwi
kama masufuria na kwa bahati nzuri serikali ikatusikiliza sisi watu
wachache tuliopinga ukodishwaji ndipo wanaposema kuwa mimi napinga
maendeleo.
“Mimi
nahitaji maendeleo ya Yanga hadi kiama lakini utaratibu ufuatwe sio
kumpa mtu mmoja, kwa kuwa viongozi wangu walitaka kukodisha na mimi
pamoja na serikali kupinga, ndiyo wameniambia mimi napinga maendeleo,
jambo hilo si sawa,” alisema Akilimali.
Post a Comment