
Waajili nchini wametakiwa kulejesha kwa wakati makato ya
wafanyakazi wao kwenye bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya
juu kwani kufanya hivyo itawasaidia wanafunzi waliokua vyuoni kuendelea kupata mikopo kwa wakati na
hata kuanza masomo yao kwa wakati maalumu pasipo usumbufu wowote.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi msaidizi urejeshaji mikopo
kutoka katika bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu(HESLB)Bw.FIDERISI
JOSEPH alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa katika kampeni ya kutembelea makampuni na taasisi
mbalimbali ambazo bado hazija rejesha
madeni ya makato wanayo daiwa
na bodi hiyo.
Amesema kuwa waajili wengi wamekuwa wakiyadhalau makato hayo na hata kushindwa kuyawasilisha kwa
wakati katika bodi hiyo hivyo hali hiyo husababisha madeni hayo kuongezeka katika makampuni
mbalimbali na kupelekea serikali
kushindwa kua na fedha za kutoa mikopo
kwa wanafunzi wanaoingia vyuoni pindi wahitajipo mikopo hiyo.
Pia FIDERISI ametoa ufafanuzi juu ya kampeni inayofanywa na bodi hiyo ya
kutembelea makampuni na taasisi niya
miezi mitatu na kwa sasa inafanyanyika Jijini DAR ES SALAAM kwa mwezi moja na
mienzi itakayo bakia itaanza kuzunguka katika mikoa minginea hapa nchini
lengo nikuwakumbusha na kutoa elimu
waajili kulipa makato kwa wakati na muda walipangiwa.
Aidha ametoa wito kwa makampuni na taasisi zote hapa nchini
ambazo hazijawasilisha makato wanayo
daiwa na bodi hiyo kuyarejesha mapema
makato hayo kwani yapo kisheria
na asiye fanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria na hata kulipishwa faini au
kifungo cha miaka mitatu.
Post a Comment