0






 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjcYHA_ED9Djgvo6zrf3TpefEWracU9HXbPHzeeT1FlnvLQW3WIW8frg6Vn_75yxA1YEd_YE36o4-fKUd0Vr5lipxGlLC-2rPhiaUPr5INhqnW1qwATFkVJcrJ6-CRXzvPmrlIUyjmhixE/s640/Screenshot_3.png









Serikali ya  Tanzania kupitia wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto leo imeungana na mataifa mengine ulimenguni kote katika  kuhadhimisha  siku ya ukoma Duniani siku hiyo inafanyika kila jumapili ya mwisho wa mwezi januari ulimwenguni kote.

Akizungumza na waandishi wa habari naibu waziri wa Wizara ya  Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto  Dkt.FAUSTINE NDUGULILE kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo amesema kuwa kwa mwaka huu siku hiyo imehazimishawa leo katika makao makuu ya wizara hiyo Jijini DAR ES SALAAM.

Pia maadhimisho hayo yanatumika   kama njia ya kuelimisha na kuongeza uelewa duniani kuhusu ugonjwa huo wa kale ambao unatibika na mgonjwa kupona kabisa vile vile Dkt.NDUGULILE ameeleza kwamba nchi yetu ilifikia viwango vya kitaifa katika kutokomeza ukoma mnamo mwaka 2006 kwa kiwango cha chini ya mgonjwa mmoja kati ya watu 10,000 lakini ungonjwa huo bado umeendelea kuwa tatizo la kiafya miongoni mwa jamii mbalimbali hapa nchini.

Hivyo basi serikali kwa kulitambua hilo inatumia njia mbalimbali katika kudhibiti ugonjwa huo hapa nchini ikiwemo kuendesha kampeni za uibuaji wa wagonjwa wapya ngazi ya jamii kwa kushirikiana na watoa huduma katika ngazi hizo pia utekelezaji wa mpango wa majaribio ya utohaji wa dawa kinga katika ngazi ya kaya kwaajili ya kuzui maambukizi ya ungonjwa huo.

Aidha naibu waziri huyo ametoa wito kwa wazazi na walezi kujijengea tabia ya kuchunguza miili yao na ya watoto wao ili kungundua kama wanadalili za ungonjwa huo  na endapo mzazi au mlezi atagundua kuwa yeye au mtoto anadalili za ukoma hivyo anatakiwa kuwai au kumuwaisha muathirika wa ungonjwa huo  mapema katika vituo vya afya ili kupatiwa matibabu kwani ugonjwa huo unatibika bure na dawa zinatolewa bure katika vituo vyote vya Afya hapa nchini.

Post a Comment

 
Top