Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema upelelezi dhidi ya
aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake umekamilika.
Awali
Mahakama ya Kisutu ilitaka Malinzi, katibu mkuu wa zamani wa TFF,
Mwesigwa Celestine na aliyekuwa mhasibu wa shirikisho hilo kuhojiwa tena
na Takukuru.
Hivyo
Takukuru imeiambia mahakama hiyo kwamba tayari upelelezi huo katika
kesi inayowakabiri Malinzi na wenzake kwa tuhuma za utakatishaji fedha
imekamilika.
Malinzi na wenzake wako mahabusu tokea mwaka jana huku kesi hiyo ikiendelea kuunguruma katika mahakama ya Kisutu.
Post a Comment