
\Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya Zara ya kukagua Maendeleo ya
Ukarabati wa Mabasi 11 ya Vyombo vya ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la
Police, Magereza na Jeshi la Wananchi ambapo hadi Mwishoni mwa mwezi
huu baadhi yatakuwa yamekamilika na kukabidhiwa.
Magari hayo ni yale
yaliyopelekwa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani yakiwa Chakavu (Screpa) na
sasa yapo katika hatua ya mwisho kukamilika yakifungwa vifaa vya kisasa
ikiwemo AC, Chaji ya Simu, TV, Viti, Bodi mpya, Taa, Side mirrors,
Tairi, Vioo huku baadhi zikiwekewa Vyoo vya Ndani.
RC Makonda ameeleza
kuridhika na kasi ya ujenzi huo ambapo ameshukuru kiwanda cha Dar Coach
Ltdkwa uzalendo wa kujitolea kukarabati Magari hayo.
Aidha RC Makonda amesema
maboresho ya Magari hayo 11 yameisaidia Serikali kuokoa kiasi cha Zaidi
ya Shillingi Billion moja ambazo serikali ingetumia lakini kampuni hiyo
imejitolea kukarabati Magari hayo Bure.
Nao Viongozi wa Vyombo
vya Ulinzi na Usalama walioambatana na RC Makonda akiwemo Kamanda wa
Polisi Kanda maalumu ya Dsm Lazaro Mambosasa, Mkuu wa Jeshi la Magereza
DCP Agustin Mboje na Kaimu Mkuu mkuu wa Usafirishaji JWTZ Canal Benjamin
Kisinda wamempongeza RC Makondakwa ubunifu anaoufanya ambapo wamesema
Magari hayo yatasaidia kuimarisha ulinzi na usalamapamoja na kuwafanya
Askari kufanya kazi katika mazingira mazuri.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa kiwanda cha Dar Coach Ltd Bwana Manmeet Lal
amemuhakikishia RC Makondakuwa magari Matano Kati ya 11 yatakabidhiwa
mwishoni mwa mwezi huu.
Post a Comment