
Baraza la taifa la usalama barabarani
limewataka wamiliki wa magari binafsi kupelekeka magari yao katika vituo vya
polisi na maeneo yaliyotegwa kwa ajili ya ukaguzi pindi ifikapo tarehe moja
march mwaka huu kwani kufanya hivyo itasaidia kupunguza ajali za barabarani
hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi na mwenyekiti wa baraza hilo mhandisi HAMAD MASAUNI alipokuwa
akitoa taarifa ya tathimini ya utendaji na utekelezaji wa awamu ya pili ya
mpango mkakati wa baraza la taifa la usalama barabarani wa kupunguza ajali za
barabarani kwa asilimia 10 katika kipindi cha miezi sita kuanzia julai hadi
desemba 2017.
Amesema kuwa tamko hilo limetoka ikiwa ni baada
ya baraza hilo kujilizishwa na mafanikio yaliyopatikana na utekelezaji wa mpango mkakati wa awamu ya pili wa kupambana na ajali za barabarani kwakufanya ukaguzi wa
magari ya biasahara,abiri na yakubebea mizigo hivyo ni vyema wamiliki wa magari
binafsi wakalitii agizo hilo pasipo shuruti.
Aidha Ametoa wito kwa kampuni zinazouza
pikipiki hapa nchini kuacha kuuza pikipiki zilizosajiliwa kwa majina ya kampuni
zao kwani kitendo hicho ni kinyume
cha sheri na kimekuwa kikisababisha usumbufu mkubwa
wakati wa ukamataji wa pikipiki zinazokamatwa kwa uvunjifu wa sheria za
barabarani na makosa mbalimbali.
Post a Comment