Wananchi pamoja na sekta mbalimbali hapa
nchini wametakiwa kutambua kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano(TEHAMA)ni
moja kati ya vitu vinavyo changia katika ukuaji wa maendeleo hapa nchini hivyo
ni vyema wakaitumia vizuri ili iwasidie katika kujiingizia kipato na hata kuwaondoa katika umaskini.
Hayo yamesemwa na Mkurugezi wa tume ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) SAMSON MWELA alipokuwa akifungua
mkutano wa jukwaa la tahama salama Tanzania (CYBERTZ) uliyofanyika Jijini DAR
ES SALAA.
Amesema kuongezeka kwa matumizi ya tehama hapa nchini imeleta mchango mkubwa
katika maendeleo ya jamii na kiuchumi kwani imesaidi kuwaunganisha wananchi
katika maeneo mbalimbali na huduma za kifedha na mabenki hivyo ni vyema wakatambua kuwa tehama ni sehemu muhimu
katika maisha yetu ya kila siku na usalama wake ni muhimu kwa ustawi.
Pia ameeleza changamoto mbalimbali
zinazosababishwa na matumizi yasiyo rasmi ya Tehama hapa nchini ikiwa ni pamoja
na maudhi yasiyo endana na maadili ya kitanzania,watu kutumia mitandao
kuchafuana,wizi na hujuma kwa njia ya mitandao na udukuaji wa taarifa kinyume
na taratibu.
Aidha ametoa wito kwa wadau wa jukwaa la
tehama salama Tanzania walioshiriki katika mkutano huo kuendelea kuwa na
ushirikiano na kubadilishana uzoefu walio nao ili kulifanya jukwaa hilo lizidi
kusonga mbele na kuendelea kutetea masilahi ya Teknolojia ya habari na
mawasiliano hapa nchini.
Post a Comment