Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya maliasili na utalii
imekutana na serikali ya china ili kujadili jinsi ya kukuza maendeleo katika
sekta ya utalii baina ya nchi hizo mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini DAR ES SALAAM katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii meja jenerali GAUDENCE
MILANZI amesema kuwa Tanzania na China zinashirikiana katika mambo mbalimbali ambayo
yanapelekea nchi zote mbili kupata maendeleo kupitia ushirikianao huo.
Hivyo basi katika kuendelea kuimalisha ushirikino huo
serikali ya Tanzania kupitia wizara ya
maliasili na utalii ikaamua kukutana na nchi ya China ili kujadili njia zitakazo ifanya sekta ya
utalii iweze kutangazika kitaifa na hata
kimataifa kwa lengo la kuifanya sekta hiyo ikue kimaendeleo hapa nchini na hata kupelekea
ukuaji wa uchumi uzidi kuongezeka.
Pia Jenerali MILANZI ameeleza kuwa majadiliano hayo
yamelenga kulikumbusha Taifa la china kuwahamasisha wananchi wake kuja wingi hapa nchini kwajili ya
kufanya utalii kwani kumekuwa na watalii
wachache wanao toka katika taifa hilo hivyo kupitia majadiliano hayo
yatapelekea kupata watalii wengi kutoka
nchini humo.
Aidha nae balozi wa china hapa nchini Bi.WANG KE amesema
kuwa nchi ya China itaendelea kuisaidia kwa nguvu serikali
ya Tanzania katika kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa kimaendeleo na pia wataakikisha kuwa wanapiga vita
ujangili nakutoa elimu kwa jamii ya china iliyopo nchini Tanzania juu
ya kuwalinda wanayapori dhidi ya ujangili.
Post a Comment