0







 

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVWsR9wisEa6tvpUaJSSCBkcueaYRMafRHldeAMufQPIgIlU5h8VFaGrhhYjWPd-Vj_W7u-0xdHHkNqRV66bgICjpYElT-ebCr-yd_F86f2goZx-0tYw_3XqG94BYgTS-2AyWMYXOsP3xx/s640/Bureau-De-Change.jpg
 Juni mwaka jana,wamiliki was maduka ya kubadilishia fedha za kigeni  walitangaziwa na  Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuwa wanatakiwa kuomba upya leseni za maduka ya kubadilisha fedha na hatua hiyo ilitokana na tuhuma mbalimbali za maduka hayo ikiwamo ya kwamba kuna baadhi ya maduka yanatumika katika utakashiji fedha.
Akizungumza mchakato kuhusu utoaji upya wa leseni kwa maduka hayo , Meneja wa Huduma za Fedha na Maduka ya kubadilisha fedha chini ya Usimamizi wa Idara ya Mabenki, Eliamringi Mandari amefafanua kuwa watatoa taarifa rasmi kuhusu mchakato huo.
Amesema kwamba  wakati mchakato wa kutoa upya  leseni kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ukiendelea, maduka yaliyokidhi  vigezo hadi sasa ni 71 na matawi 40 kati ya maduka 297 yaliyokuwepo awali.
Mandari amesema hayo wakati akitoa  mada inayohusu kanuni mpya za usimamizi wa maduka ya fedha kwa waandishi wa habari waliopo kwenye semina iliyoandaliwa na BoT.
“Naomba hapa tuelewane kwanza,mchakato wa kutoa leseni kwa maduka hayo ya kubadilisha fedha za kigeni bado unaendelea na utakamilika siku za karibuni na baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi.
Lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wa taarifa sahihi zinazohusu uchumi,biashara na fedha,ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kati ya maduka hayo 297ni maduka 71 tu ndio yamekidhi vigezo.
“Hii taarifa ambayo tunaieleza si kwamba ndio taarifa ya mwisho ila naelezea hatua ambayo tumefikia hadi sasa.Mchakato huo ulianza Juni mwaka jana na ulitakiwa kukamilika Desemba mwaka jana.
” Mchakato umechelewa kutokana na wamiliki wa maduka wengi walichelewa kuleta maombi tarehe 29 ya Desemba mwaka jana.Hivyo tumefunga maombi ya leseni na kinachoendelea no kupitia maombi maduka 65 na tukimaliza ndio tutatoa taarifa rasmi,”amesema Mandari.
“Maduka 297 ya kubadilisha fedha za kigeni ndio yalikuwepo lakini kutokana na mchakato unaoendelea wapo walioshindwa kutimiza vigezo vilovyowekwa.Matokeo yake maduka yaliyokidhi vigezo ni 71 na matawi 40,hivyo tunaweza kusema ni kama maduka 111,” amesema Mandari.
Akifafanua zaidi Mandari amesema hadi sasa maduka ambayo yamekidhi masharti na vigezo vilivyotolewa na BoT ni 71 pamoja na matawi 40.Wamiliki wengine wa maduka hayo wapatao 50 wameshindwa kuomba maana hawajasema chochote ila wameona wapo kimya.
.Ameongeza kwa kuwa muda wa maombi ulishakwisha maana yake hata kama maduka 65 ambayo maombi yake ndio yanaendelea kupitiwa hata kama yote yatapita bado idadi ya maduka haitafikia ile ya mwanzo kwani yamepungua.
Alipoukizwa maduka ambayo yamefungwa wameshindwa katika vigezo gani,amejibu wapo walioshindwa kwasababu ya kushindwa kuelezea mtaji wa fedha zao ,kwani wapo ambayo wamesema wamesema mitaji yao ilitokana na kuuza mali zao.

Post a Comment

 
Top