
Na.Martin joseph
Watanzania pamoja na wadau mbalimbali nchini wamekumbushwa kulinda,kuhifadhi na kuendeleza
historia ya ukombozi wa bara la Africa ili kukuza na kuleta tija hapa nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe
ameyasema hayo leo wakati akifanya ziara ya kutelembelea Jengo la Makumbusho ya
Ukombozi wa Bara la Africa jijini Dar es
salaam.
Dkt Mwakyembe amesema Tanzania imepewa jukumu zito na Umoja wa Afrika
kuhakikisha wanasimamia na kuhifadhi historia ambazo zimesababisha ukombozi wa
bara la Afrika.
Kwa Upande wake Msimamizi Mkuu wa mradi wa Urithi wa ukombozi wa Bara la
Afrika bi,Ingiahed Mduma amesema wanatarajia kutengenezaneza mradi mkubwa wenye
lengo la kuitangaza Tanzania kupitia utalii.
Jengo hilo ambalo ndio makao makuu ya Kamati ya Ukombozi ya OAU ilianza
mwaka 1969 baada ya kamati hiyo kukamilisha jukumu lake la ukombozi wa bara
ziuma la Afrika na hivyo mnamo Novemba 4,1994 lilikabidhiwa kwa JWTZ ili
litumike kama makumbusho ya Historia ya Jeshi pamoja na makumbusho ya Ukombozi.
Post a Comment