
Na.Chanzo Chetu cha habari
Baada ya kukosa michezo mitatu mfululizo
kutokana na kupata majeraha, nahodha na kiungo wa Azam FC, Himid Mao,
huenda akapelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Kiungo huyo alikosa mchezo dhidi ya
Simba hivi karibuni ambao timu yake ilipoteza kwa bao 1-0 katika Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Daktari wa timu hiyo, Mwanandi
Mwankemwa, alisema kuwa kiungo huyo ana tatizo la goti na amekuwa
akitibiwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi).
Aidha alisema kutokana na hali hiyo na maendeleo yake baada ya vipimo anatarajiwa kuwasilisha suala hilo kwa uongozi ikiwezekana kwenda kutibiwa Sauz.
“Himid bado kuweza kurejea uwanjani
kutokana na tatizo la goti ambalo kwa sasa linamsumbua na anatibiwa
katika Taasisi ya Mifupa, Moi na kutokana na jinsi alivyo sasa
tunasubiri vipimo kisha nitapeleka kwenye bodi ya timu kuweza kupelekwa
Afrika Kusini kwa matibabu.
“Kwa sasa hana uwezo wa kurejea uwanjani kutokana
na hilo tatizo, pale atakapokuwa fiti na akatibiwa kabisa wakati
ukifika hilo tutaweza kuwaeleza pia,” alisema Mwankemwa.
Post a Comment