0











 https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/7169/production/_99933092__99921339_c390954a-c6e0-4aaf-8070-ac16ed2abcca-1.jpg



Umoja wa mataifa umetoa wito kusitishwa kwa mapigano hayo mapema iwezekanavyo.Awali majeshi ya Syria yalidai kuwa vikosi vya anga vya Israel vilishambulia ngome za kijeshi zilizopo karibu na mji mkuu Damascus.

Taarifa kutoka BBC zinasema Raia mmoja wa kutoka eneo la Douma nje kidogo ya Damascus ambaye hakutaka kutajwa jina lake ameiambia juu ya hali ilivyo kufuatia mashambulizi hayo
"Tuna raia 19 waliojeruhiwa.Nyumba zimeharibiwa vibaya kutokana na mashambulizi haya ya anga,ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya kumi hapa wakiwemo akina mama na watoto.Hapa Douma pekee yake tangu kuanza kwa mashambulizi haya watu 33 waliouawa,ukiongeza na wengine 19 waliouawa al-Ghouta.Tuna maji na chakula lakini tatizo ni huduma za dawa.Tuna Zaidi ya majeruhi 700 hapa wanaohitaji huduma ya haraka ya afya,wanaweza kufa muda wowote.''.

Vikosi vya uokoaji mashambulizi hayo ya anga yamelenga maeneo kadhaa katika miji ya mashariki mwa Ghuta kuanzia hapo jana,hali inayosababisha makazi ya watu kubomoka.
Zaidi ya watu 130 hadi sasa wanahofiwa kufa tangu vikosi vya serikali ya Syria vilipoanzisha mashambulizi ya anga siku ya jumatatu wiki hii. Zaidi ya raia 400,000 wapo katika eneo la mapigano Mashariki mwa mji wa Gouta tangu mwaka 2013.

Post a Comment

 
Top