
Shirika lisilo la kiserikali la Hakielimu limeiomba serikali
kuwawekea mazingira mazuri wanafunzi wenye changamoto ya uoni mashuleni kwani
kwakufanya hivyo itawasaidia wanafunzi hao kupata elimu iliyo bora na itakayo
wasaidia katika maisha yao na hata kuondokana na utegemezi wa watu mbalimbali.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo la HAKIELIMU JOHN KALAGE alipokuwa Jijini DAR
ES SALAAM katika mkutano wa uzinduzi wa tathimini ya mafunzo na ushirikishwaji
wa wanafunzi wenye changamoto ya uoni katika shule jumuishi hapa nchini.
Amesema kuwa mazingira mabovu kwa wanafunzi hao yamekuwa
yakiwapa shida sana na hata muda mwingine kuwapelekea kushindwa kupata elimu
iliyo bora ambayo ingewasaidia katika maisha yao na hata kuzifanya familia zao kupata maendeleo.
Pia ameeleza changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye
changamoto ya uoni mashuleni ikiwa ni pamoja na upungufu wa walimu wenye ujuzi
wa kuwafundisha wanafunzi hao,kushindwa kutembea katika maeneo ya shule kutokana
na miundombinu isiyo rafiki na kuwanyanyapaa wanafunzi wenye changamoto za uoni
kutoka kwa baadhi ya walimu na hata kwa wanafunzi wenzao.
Aidha KALAGE ametoa wito kwa wadau mbalimbali,taasisi na
mashirika kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto zinazo wakabili
wanafunzi wenye changamoto ya uoni ili kuwafanya waweze kufika mbali kielimu na
hata waweze kuondokana katika tatizo la utegemezi na waweze kujitegemea
wenyewe.
Post a Comment