Hayo yamesemwa na
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. HARRISON MWAKYEMBE alipokuwa
katika mkutano na waandishi wa habari Jijini DAR ES SALAAM akitoa ufafanuzi
kuhusu ujenzi wa kituo kikuu cha
kumbukumbu ya ukombozi wa bara la Afrika kinachotalajiwa kujengwa katika eneo
la MWABEPANDE Jijini DAR ES SALAAM.
Amsema histori ya Afrika inawategemea Waafrika wenyewe hivyo
ni vyema Watanzania wakatambua kuwa ni muhimu kuisimamia vyema historia hiyo
ili isaidie kwavizazi vinavyokuja na wajue kuwa
walipotoka ni wapi na
wanapokwenda ni wapi kwani hii itakua faida kubwa katika maisha yao.
Pia kwa upande mwingine waziri MWAKYEMBE ameushukulu ubalozi
wa URUSI pamoja na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP)
kwakukubali kushirikiana na serikali
katika kufanikisha mradi huo ambao utasaidia katika kutunza historia mbalimbali
za Afrika pamoja na zile za Tanzania.
Aidha ametoa wito kwa wananchi hasa hasa vijana kuvitumia
vivutio vilivypo hapa nchini ambavyo vimetumza historia mbalimbali kama fursa ya kujipatia kipato kwa watu
watakao jitokeza kutembelea maeneo hayo kwa lengo la kufanya utalii.
Post a Comment