
Serikali kupitia ofisi ya taifa ya Takwimu imetoa takwimu
ya mfuko wa bei za bidhaa katika Taifa
kwa mwezi Desemba mwaka jana pamoja na mwezi Januari mwaka huu ambapo imeelezwa
kuwa kasi hiyo imebaki kuwa sawa ambapo mwezi januari mwaka huu emebaki kuwa asilimia 4 ambapo ukilinganisha
na hile ya mwezi desemba mwaka jana.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa sensa na takwimu za jamii kutoka
katika ofisi za Taifa ya Takwimu(NBS)EPHIAM KWESIGABO alipokuwa akitoa taarifa
kwa vyombo vya habari Jijini DAR ES
SALAAM kuhusu kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya
binafsi nchini.
Amesema kuwa hali hiyo imebaki kuwa hivyo kutokana na kazi
kubwa inayofanywa na serikali ya kuhakikisha
kuwa miradi mbalimbli ambayo
ilikuwa ikichangia mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nyingine kuongezeka hivyo
nivyema wananchi wakaendelea kuiunga mkono
serikali katika kuhakikisha bei za bidhaa hapa nchini inakuwa nzuri.
Aidha KWESIGABO ameeleza baadhi ya bidhaa za vyakula
zilizochangia mfumuko wa bei kufikia asilimia 4 kwa mwezi januari mwaka jana na
mwezi januari mwaka huu ambapo mahindi kwa asilimia 8,Maharage kwa asilimia
4.3,Samaki kwa asilimia 9 na ndizi za kupikia kwa asilimia 9.
Post a Comment