0




































 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdoNLVvT4AGGXKEVsk_FANvBLEGZoU6TQ1cjKU-wzxQeNIGiU4ILOrHcWnuvkv96wxxBY-k2qoUEfzgXKczvzyQTz7uZWLch1i0VEDKDJceDgjdNh05daxKv2te8XGk5yMA5rWOag-k3vI/s640/02.JPG

Wakulima nchini wametakiwa kushiriki katika semina na mikutano  mbalimbali inayo husika na maswala ya kilimo kwani kufanya hivyo itawasaidia kupata fursa  na ufahamu wa kujua  njia za   kujikwamua kupitia kilimo.
 Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa mtandao wa kijani kibichi Tanzania (MKIKITA) ADAM NGAMANGE alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Jijini DAR ES SALAAM kuhusu mkutano wa kutoa mafunzo kwa wakulima ulioandaliwa na Mtandao huo kwakushirikiana na taasisi inayojishugulisha na utoaji wa mafunzo kwa wakulima(ALL FOR ALL FOUNDATION) unaotalajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu Jijini DAR ES SALAAM.
Amesema kumekuwa na wakulima wachache wenye uelewa kuhusu kilimo bora na chenye manufaa hivyo hali imekua ikipelekea uzalishaji wa mazao kuwa mdogo na hata kuwafanya  wakulima wengi  kuwa maskini kutokana na kukosa njia ambazo zingewasaidia kuondokana na tatizo hilo ambalo limekuwa likiwakabili wakulima wengi hapa nchini.
Hivyo basi  Mtandao wa kijani kibichi kwa ushirikiana na taasisi inayojishugulisha na kutoa mafunzo kwa wakulima wakaamua kuanzisha mafunzo hayo kwa lengo la kuwasaidia wakulima kujifunza mambo mengi ya kilimo ili kuboresha kilimo kwa kila mkulima aliyekuwa hapa nchini  ili iwasaidie katika kupata  maendeleo yao binafsi na hata ya taifa kwa ujumla.
Aidha NGAMANGE ameiomba serikali iendelee kushirikiana na watu binafsi pamoja na mitando mbalimbali inayojishugulisha na maswala ya kilimo ili kuwasaidia wakulima  kulima kilimo bora na kupata masoko mazuri ambayo yatawafanya wakulima kuuza bidhaa zao kwa uraisi na kupata kipato kitakacho wasaidi na hata kuondokana na wimbi la umaskini.

Post a Comment

 
Top