Wakati michuano ya Kombe la Dunia
2018, ambayo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya Coca-Cola inakaribia
kuanza,kampuni ya kutengeneza vinywaji ya Nyanza Bottlers leo imezindua
promosheni itakayotoa fursa kwa wateja wake kujishindia luninga za
kisasa, zitakazowezesha kufaidi uhondo wa michuano ya kombe la dunia
wakiwa majumbani kwao.
Promosheni hii ambayo inajulikana
kama ‘ Mzuka wa Soka na CoKa’ itawahusu watumiaji wa soda za Coca-Cola,
Sprite, Fanta, Sparleta na Stoney Tangawizi katika mikoa ya Kanda ya
ziwa .
Mbali na zawadi za
televisheni,watumiaji wa vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola, kupitia
promoheni hii wataweza kujishindia zawadi nyinginezo mbalimbali ikiwemo
,fedha taslimu kati ya shilingi 5,000 mpaka shilingi 100,000/-kofia, t
shirt,soda za bure na zawadi kubwa ya bodaboda.
Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni
ya Nyanza Bottlers,Samwel Makenge ,amesema Coca-Cola ikiwa ni mdhamini
mkuu wa mashindano ya Kombe la Dunia 2018,imekuja na promosheni ya
kuleta shangwe za mashindano hayo katika mkoa wa Mwanza,utakaowawezesha
wateja wake kufurahia mashindano haya ya soka makubwa duniani wakati
huohuo wakiburudika na vinywaji vya Coca-Cola na kujishindia zawadi
kemkem.
“Wakati michuano ya Kombe la
Dunia inakaribia kuanza,tumeona tuje na promosheni hii ambayo itawezesha
watumiaji wengi wa vinywaji vya kampuni yetu kujisindia luninga za
kisasa aina ya SONY LED zenye kioo cha mbele bapa ili wapate uhondo wa
mashindano hayo.Kinachotakiwa ni kunywa soda na kushinda zawadi”.Alisema
Makenge.
Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Nyanza
Bottler,Japhet Kisusi,alisema ili kujishindia zawadi anachotakiwa
kufanya mtumiaji wa soda ni kuangalia ganda la chini ya kizibo baada ya
kunywa soda linakuwa na picha ya zawadi aliyobahatika kujishindia. “Kwa
upande wa zawadi ya pikipiki anachotakiwa kufanya mteja ni kuunganisha
picha tatu vinavyokamilisha picha ya pikipiki kutokana na ganda
atakalokuta ndani ya soda.kuna sehemu ya mbele,kati na nyuma.Zawadi zote
kubwa zitachukuliwa kiwandani na ndogo kama kofia,T shirt na soda za
bure zitatolewa na mawakala wa kampuni waliosambaa maeneo
mbalimbali”.Alisisitiza.
Kwa upande wake,Meneja wa Chapa
ya Coca-Cola nchini,Sialouise Shayo,alisema promosheni hii inadhihirisha
dhamira ya kampuni ya kuwawezesha wateja wake na watanzania kwa ujumla
kupata ‘Mzuka wa Soka na Coka’ katika msimu wa kombe la Dunia na
kujisikia sehemu ni sehemu ya mashindano hayo.
Katika maandalizi ya Mashindano
ya Kombe la Dunia 2018,Coca-Cola imetangaza hivi karibuni kuwa msanii
mmoja wa Tanzania atashirikiana na mwanamziki nguli wa kimataifa, Jason
Derulo ,kutengeza wimbo maalumu wa mashindano hayo wenye vionjo vya
Tanzania.
Post a Comment