Na.Martin Joseph
Meya wa Jiji la DAR ES SALAAM ISAYA MWITA amemtaka mkurugenzi wa jiji hilo Bi.SPORAH
LYANA pamoja na kamati yake kusimamia na kurekebisha bajeti pamoja na makusanyo mbalimbali kwani
kwakufanya hivyo kutasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ndani
ya jiji hilo.
Meya huyo ameyasema hayo Jijini DAR ES SALAAM wakati akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kumaliza kikao cha kupitia taarifa mbalimbali zilizo wasailishwa na
wanakamati waliochanguliwa na baraza hilo.
Amesema kuwa ukusanyaji
mapato na mambo mengine katika Jiji hilo yanakwenda Vizuri kwani mwaka wa fedha wa serikali uliyoisha mwezi
oktoba mwaka jana walikusanya asilimia 54
ya bajeti yote zilizopangwa na serikali kwaiyo wanatalajia mbaka ikifika mwaka
mpya wa serikali unaoanza mwezi july mwaka huu wanaweza wakaweka rekodi katika
upande wa ukusanyaji mapato na bajeti yote kwa ujumla hivyo ameeleza kuwa
katika kuyatimiza hayo nivyema ukusanyaji wa mapato ukasimamiwa vyema ili
malengo hayo yeweze kutimia.
Pia ameeleza kuwa katika juhudi za kufanya ukusanyaji
mapato unaongezeka katika jiji hilo wamehamua kuziwekea kipaumbele shuguli za utalii
kwani kwasasa wanavisiwa ambavyo vinatumika kwa shuguli hizo na pia wanatajia
kuongeza wanyama ambao watatumika katika kuwavutia watu kufanya utalii kwa
asilimia kubwa jijini hapo na kufanya mapato yazidi kuongezeka.
Aidha amezitaka halmashauri zote za Jiji la DAR ES SALAAM
kuwasajili watu watakao tumika kwajili ya kuzika watu
wasio kuwa na ndugu kwani kwasasa sheria inawaruhusu kufanya hivyo kwa mtu yoyote yule ambaye amekumbwa
na matatizo hayo.
Post a Comment