
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewahimiza wazazi hasa wanaccm kuwapa malezi bora watoto wao na kuwafunza kuwa na nidhamu.
Hayo yalisemwa na
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ( NEC) Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa ( SUKI) Ndugu Ngemela Lubinga wakati wa ziara yake Mkoani
Songwe tarehe 19/03/2018 hadi 22/03/2018.
Aliwaeleza kwamba nidhamu na malezi bora ndio njia pekee ya kujenga jamii bora inayotambua na kutekeleza wajibu wake.
Jamii bora ndio
msingi wa maendeleo ya Taifa letu hasa wakati huu wa Serikali ya awamu
ya tano chini ya mheshimiwa Rais Dokta John Magufuli inayotoa msukumo
katika uwajibikaji ili kulivusha taifa letu kufikia uchumi wa katiLubinga aliwaeleza kwamba sheria haiwezi kufanya kazi vizuri
kama hakuna malezi bora yanayoanzia katika ngazi ya familia.
Aidha
aliwaeleza kuwa matatizo yanayotokea hata katika watumishi wa Serikali
kuwanyanyasa na kutowatendea haki wananchi inatokana na kukosa malezi
bora kwani watumishi hao hawaanguki kutoka juu bali wamezaliwa na watu.
Pia aliwaasa vijana kuzingatia malezi na kutokubali kushawishiwa
kushiriki katika vitendo vya uvunjifu wa amani kama maandamano na
vurugu. Alihitimisha kwa kugawagawia jezi na mipira vijana wa kijiji cha
itumbula wilayani Momba.
Post a Comment