
Wananchi
wameombwa kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kuchangia damu ili waweze kuchangia damu hasa kipindi hiki cha
chakuelekea sikuu ya pasaka kwani bado kumekuwa na wahitaji wengi wa damu
katika hospitali mbalimbali hapa nchini.
Hayo yameelezwa na Afisa Mhamasishaji kutoka wizara Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bi.FATMA
MJUNGU wakati akizungumza na waandishi
wa habari katika zoezi la uchangiaji wa damu lililikua likifanyika eneo la Kariakoo Jijini DAR ES SALAAM.
Amesema kumekuwa
na changamoto kubwa kutokana na kutokuwa na muitikoa wa watu wengi kujitokeza
kuchangia damu hususani kwa wanawake hivyo hali hiyo imekua ikipelekea kuwepo
kwa uchache wa damu katika vitu vya afya mbalimbali na hii imekua ikisababisha watu
kushindwa kupata damu kwa wakati pale wanapohitaji.
Pia ameeleza kuwa mahitaji ya damu kwasasa
yamekuwa ni mengi hasa kwa
watu wanaofanyiwa upasuji hivyo upungufu
wa damu katika vituo vya afya unaweza ukapelekea watu hao kupoteza
maisha kwasababu zisizo kuwa za msingi.
Aidha kwa upande
mwingine nae mmoja katika ya watu
waliojitokeza kuchangia damu katika eneo hilo HASSAN SAID amesema kuwa swala la
kuchangia damu ni sehemu ya kutoa sadaka kama unavyo toa sadaka nyingine kwa
kuokoa maisha ya watu hivyo nivyema wananchi wakatambua kuwa ni muhimu
kuchangia damu ili kuokoa maisha ya
watu.
Post a Comment