0


Image result for kichere tra

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) leo imezindua Rasmi mfumo wa utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo ambao wapo kwenye sekta hiyo wakiwemo wamachinga.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliyofanyika Jijini DAR ES SALAAM Kamishina wa mamlaka hiyo CHARLES KICHERE amesema kuwa utohaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara hao unatokana na marekebisho ya sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 yaliyofanyawa na kikao cha bunge la bajeti la mwaka wa fedha 2017/18 ambapo moja ya marekebisho hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho maalum wafanyabishara wadogo.
Pia ameeleza kuwa zoezi hilo linatekelezwa na mamlaka ya mapato Tanzania kwa kushirikiana na mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(TAMISEMI),Wakala wa usajili,Ufilisi wa Udhamini(RITA) pamoja na Idara ya uhamiaji.
Aidha ametaja njia ambazo wafanyabishara wadogo wanahitajika kuzitumia pindi wanapohitaji vitambulisho hivyo maalum ikiwemo kujiunga katika vikundi maalum vinavyotambuliwa kisheria na serikali,kuwa na kitambulisho cha Taifa,kuwa na namba ya Utambulisho wa Mlipakodi ya vikundi wanavyojiunga pamoja na kuchangia shilingi elfu 10,000.

Post a Comment

 
Top