0

 
 
 
 
 
Tafadhari rejea mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mnamo tarehe 8/03/2018 katika ukumbi wa Mwl J.K Nyerere, uliohitishwa na Mweshimiwa Dr. Harrison G . Mwakyembe. 

Kwanza kabisa pokeeni Shukrani kutoka kwa Kamati kuu ya Taasisi Hii ya kimataifa ya Wataalamu wa Lojistiki na Usafirishaji kwa mwitikio wenu.

Tayali Raisi wa Taasisi na Katibu Mkuu wamesafiri Kwenda Nigeria kuhudhuria mkutano hou wa Afrika pamoja na wajumbe wengine wanne, wanatarajiwa kurudi Nchini mnamo tarehe 17 mwezi huu. 

Tafadhali rejea kichwa cha habari, Moja ya yaliyozungumzwa siku tajwa ilikua ni pamoja na mimi mtanzania mwenzenu kukabidhiwa Cheti kama zawadi ya Kua Miongoni mwa Washindi sita Duniani wa tuzo ya mtaalamu bora kijana kimataifa katika usafirishaji na Lojistiki pamoja na washindi wengine watano ambao ni Sonia Man-yee kutoka China, Muhammad Refayet Choudhury kutoka Bangradesh, Jenna Hood kutoka Australia, Jesaya Mwadingi kutoka Namibia, na Virginia Christians kutoka Newzeland. 

Kwa kusema hayo ningependa kuambatanisha Taarifa yangu Fupi inayohusu Historia yangu na jinsi nilivyofika hapa nilipo. Ninaomba Iandikwe kwenye magazeti iwe kama Chachu ya kuonesha mwanga kwa vijana wengine wenye taaluma mbalimbali, pia nipo tayari kufanya mahojiano na katika vipindi mbarimbari vya radio na runinga, bila kusahau mitandao mingine yote ya kijamii kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.

Post a Comment

 
Top